Unaweza usikubali na ukaona kama haiwezekani, lakini ndivyo ilivyo kwamba Ndondo Cup itapigwa China baada ya balozi wa China nchini Mh. Dr. Lu Youqing kutoa ahadi hiyo wakati wa uzinduzi wa ukarabati wa uwanja wa Bandari moja kati ya viwanja vinavyotumiwa katika michuano ya Ndondo Cup.
Mh. Dr Youqing amesema, anafanya mpango baada ya michuano hiyo kumalizika, waandaaji wa mashindano wataandaa timu ya Ndondo Cup ambayo itasafiri kwenda kucheza China na timu za soka za huko.
“Baada ya mashindano haya kukamilika, tutafanya utaratibu timu ya Ndondo Cup kutoka Tanzania iende China kucheza mechi za kirafiki na timu za kule kwa ajili ya kuwaongezea ujuzi wachezaji watakaofanya vizuri kwenye mashindano haya,” Dr. Lu Youqing.
Baada msimu uliopita kumalizika, iliundwa timu ya Ndondo Cup All Stars ambayo ilijumuisha wachezaji wote waliofanya vizuri kwenye mashindano hayo. Kwa hiyo, wachezaji watakaouta Ndondo Cup All Stars ya mwaka huu ndio watakaosafiri kwenda kwenye ziara ya mechi za kirafiki nchini China.
Msimu huu utakuwa ni wan ne mfululizo wa michuano ya Ndondo Cup baada ya msimu wa tatu kumalizika huku Temeke Market wakiwa ndio mabingwa wa msimu uliopita walipoifunga timu nyingine ya Temeke Kauzu FC.
No comments:
Post a Comment