Taarifa za kuuzwa kwa timu ya African Lyon inayoshiriki ligi kuu Tanzania bara zinazidi kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba kampuni ya GSM ipo kwenye mipango ya kuinunua klabu hiyo inayomilikiwa na Rahim Zamunda.
Mmiliki wa African Lyon Rahim Zamunda amesema klabu hiyo haiuzwi taarifa zinazosambaa kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii zinatokana na uhusiano mzuri uliopo kati ya African Lyon na GSM na kama timu hiyo itakuwa inauzwa basi kila kitu kitawekwa wazi.
“African Lyon is not for sell, African Lyon haijauzwa hizo ni taarifa za kwenye mitandao ya kijamii. Tuna uhusiano mzuri na GSM ndio maana kila mtu anasema maneno yake kadiri anavyojisika kwenye mitandao ya kijamii,” – Rahim Zamunda mmiliki wa African Lyon wakati alipohojiwa na Clouds FM kwenye Hili Game ndani ya Power Breakfast.
“Kama kitu kama hicho kitatokea basi tutatoa taarifa, lakini kwa sasa African Lyon haiuzwi. Tumekuwa nah ii timu kwa miaka saba tuna mipango yetu kwa ajili ya kuiendeleza hii timu lakini kama kutakuwa na kuuzwa kwa timu kila mtu atajua.”
GSM kwa sasa ni wadhamini wa klabu ya Majimaji FC ya mkoani Ruvuma ambayo ipo kwenye ukanda wa kushuka daraja.
Inatajwa kuwa, GSM ipo tayari kuinunua klabu ya African Lyon endapo itasalia ligi kuu Tanzania bara endapo itashuka basi dili hilo litakuwa limeota mabawa.
African Lyon ipo katika nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 baada ya kucheza mechi 13 ikiwa imeshinda mechi nne tu imetoka sare kwenye mechi 11 na kupoteza michezo nane.
No comments:
Post a Comment