Kocha wa Chelsea Antonio Conte, amesikitishwa na walinzi wake kuruhusu bao la dakika za majeruhi, licha ya kikosi chake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Ham usiku wa jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya England.
Manuel Lanzini akifunga bao la kufutia machozi kwa Westham dhidi ya Chelsea dakika ya 90.
Conte amesema ni mbaya sana kuruhusu goli katika dakika za mwishoni na kuwataka wachezaji wake kujirekebisha na makosa hayo.
"Ni masikitiko kwa bao tuliloruhusu mwishoni mwa mchezo. Tulipoteza matokeo ya kutoruhusu bao kwa mara nyingine, siyo kitu kizuri. Lazima tujirekebishe na hali hii."
Edin Hazard na Diego Costa waliiweka Chelsea mbele kwa mabao yao, lakini Manuel Lanzini akafunga bao la kufutia machozi kwa West Ham katika dakika ya 90.
Sasa, baada ya mechi 27, Chelsea wana pointi 66, Tottenham 56 na wa tatu ni Manchester City wenye pointi 55 kwa mechi 26.
Anthonio Conte
No comments:
Post a Comment