Thursday, March 2, 2017

Klopp: Muda ni Tusi Kubwa Ndani ya Anfield

Generated by IJG JPEG Library
Ulikuwa kama Mwanga umeanza kuchomoza wakati msimu unaanza na Klopp alionekana kama Malaika mwokozi, kabla mechi ya Leicester haijaonyesha mahala ambapo shetani alijificha, naam Liverpool wamepoteza kwa mabao 3-1, na huwezi kuwafikiri tena kama timu inayogombea ubingwa.
Ikumbuke Liverpool ya mwezi August walikuwa jina la kwanza kabisa ambalo ungeweza kulifikiri kama klabu ambayo itatoa changamoto kwenye mbio za ubingwa msimu huu huku kiwango chao kikipanda kila kukicha.
Lakini ni kama maajabu, yaite miujiza kama moyo wako ungependa kufanya hivyo, lakini katika michezo 5 iliyopita wamepoteza mara 3 na sura ya Klopp haina tena ile haiba iliyozoeleka, na ni kama miwani yake haimruhusu kuona vile ambavyo wengi wanavitizama kwa usahihi. Inawezekana miwani yake ikamwonyesha anaweza kushiriki UEFA mwakani, lakini macho ya kawaida ya waliokuwa wengi hayatizami hilo tena.
Liverpool began the season so brightly but now it's all going wrong for Jurgen Klopp
Inawezekana Dante na Yondani walikupa Maswali mengi kwa namna waliyocheza na Mavugo, lakini Liverpool inaweza ikakupa milinganyo ambayo hakuna kikokotoleo kinachoweza kukupa majibu sahihi kwa haraka. Utatakiwa kuwa mjuzi haswaa.
Na ugonjwa huu haukuanza leo, ilitakiwa kuwa imeshapata tiba kwa sababu ilishaonekana tangu alipokuwepo Malaika Suarez kwani waliruhusu mabao 50. Huu ni ugonjwa ambao Klopp anaufahamu lakini maabara yake haijafanikiwa kuibuka na dawa ama tiba sahihi mpaka leo.
Wakati Milner anafanya vyema kwenye nafasi ya beki wa kushoto baada ya Alberto Moreno kuamua kujaribu ujinga kila akiingia uwanjani, lilikuwa suala la muda tu mpaka Milner akose hamu ya kucheza nafasi hiyo. Lakini ni huyu Klopp ambaye alijaribu kuamini katika kujituma na nguvu kazi yake Milner kuliko uwezo. Sasa inamuadhibu.
Bahati mbaya zaidi ni kuwa hata kwenye moyo wa safu ya Ulinzi yaani mabeki wa kati, hakuna muunganiko. Sio Matip ambaye anaonekana kama ana laana ya Wakameruni, sio Dejan Lovren ambaye alitakiwa awe ameondoka kabla ya Sakho na wala tiba haikuwahi kufikiriwa kuwa Lucas ambaye hana kasi tena ijapokuwa hata wakati wa ujana wake alikuwa ni kobe kijana tu. Liverpool imeruhusu magoli mengi kuliko klabu yoyote ndani ya timu 10 za juu isipokuwa Stoke City na West Ham.
Jarida la Mail la Uingereza liliwahi kuhoji uzito wa kikosi cha Liverpool baada ya sare dhidi ya Sunderland. Naam kwenye mbao ndefu kulikuwa na Stewart mwenye miaka 23, Trent-Alexander Arnold  18 na Ovie Ejaria 19.
Kwenye nyakati ambazo Coutinho amesahau viatu vyake, Henderson haeleweki matibabu yake Liverpool kama wasindani walitakiwa kuwa na silaha tofauti na Firmino na Mane peke yake.
Bahati mbaya na Mane amekuwa na nyakati ngumu, huku Firimino majukumu aliyopewa yanamfanya kutokuwa na ukali wa magoli muda mwingi, anafanya kazi kubwa mno ambayo ilitakiwa msaada kama ambavyo msimu ulianza. Lakini hili haliwezekani kama Lallana, Coutinho hawafanyi kazi yao ipasavyo huku Daniel Sturridge akiwa anauchukia mpira kabisa.
A lack of depth has seen 18-year-old Trent Alexander-Arnold often included for Liverpool
Klopp alifanya jambo sahihi kwa kuanza na usajili mdogo wa Wijnaldum na Mane ambao haukuondoa mazoea yaliyokuwepo kabla bali iliongeza wepesi lakini kwa aina yake ya mchezo na ukifikiri majeraha, kikosi cha Liverpool ni chepesi sana.
Pamoja na mbinu zake mara nyingi kuwa tofauti na makocha wengi, na ndio sababu kila kocha aliogopa kukutana naye mwanzo wa msimu, bado Klopp anabeba lawama kwa kushindwa kufahamu namna ya kumaliza mbio, ugonjwa wa muda mrefu kwenye akili ya Arsene Wenger.  Liverpool kwa sasa inacheza kama haina inachofundishwa kwenye uwanja wa mazoezi pale Melwood, ni kama haina kocha.
Klopp played Lucas at the heart of defence at the King Power, to disastrous consequences
Maisha ndivyo yalivyo, lakini Faru hajifunzi ukali wa moto mpaka afe, siku zote atarudia kuunganyaga. Pamoja na Lucas kuonekana kuwa hajawahi kuwa chaguo sahihi kwenye eneo la beki, bado Klopp aliamua kulalia ncha ya upanga na Jamie Vardy hakupata shida kumtoboa. Hili ni tatizo kwa makocha wanaoamini kuwa wana akili nyingi za kimbinu, ugonjwa wa Guardiola pia, wameweka pamba masikioni.
Na mafuriko hayawi mafuriko kama hayajaharibu miundombinu, Liverpool wamepoteza nafasi ya Ubingwa katika hili, wamepoteza kujiamini na hawaonekani kama watafuzu kirahisi kwenye timu nne za juu.
Daniel Sturridge appears to hinder the flow when tactics are switched to accommodate him
Liverpool wamekufa kiakili lakini inaonekana hata kihisia wamezikwa tayari. Imani yao kama bado ni timu bora imeondoka na wala hakuna anayewahofia tena, sababu iliyowafanya Wolves kushinda mchezo wa FA kwa staili waliyotaka wao.
Liverpool ya Klopp haijafungwa na klabu yoyote iliyokuwa kwenye timu 6 za juu, hii ni sifa ya kijana mwenye kiburi tu ambaye anaamini ana misuli inayoweza kumfanya apigane. Dhidi ya wakubwa anapania na anasahau kulinda uso wake dhidi ya wadogo, umakini unapokuwa sifuri, hasara yake ni utajiri unaopotea. Liverpool taratibu wanakuwa fukara ndani ya uwanja.
Beating struggling teams has been a constant mentality nightmare for the Reds this season
Kwa mwaka, 2017 vilabu vya Sunderland, Swansea, Hull City  na Leicester vyote vimestuka usingizini kutoka kwa Liverpool, vilabu ambavyo havifahamu majaliwa yao ya kutokushuka daraja.  Usisahau moshi ulioanza kuonyesha moto utakaowaunguza ulianza kwa Burnley kisha Bournemouth. Sasa Klopp anakaribia kuokota majivu.
Inawezekana kabisa hata wale makocha waliosema hakuna timu bora kwenye ligi kuu ya Uingereza kwa sasa kama Liverpool wakawa wanauma midomo yao kwa hasira kwa namna ambayo hawakuwa werevu.
Klopp has been repeatedly livid when the Reds have been found out and may need to reinventMuda bado upo iwapo tu Klopp ataamua kuiheshimu saa. Jina lake linashabiana na lile la mashabiki wa Liverpool yaani Klopp na Kop lakini inawezekana tabia zao zikaanza kwenda tofauti. Aliwahi kuwalaumu kwa kuwahi kuondoka uwanjani akawapa matokeo sahihi wakatulia, sasa akiendelea hivi watakimbia kabisa. Wale mashabiki wa enzi za Bill Shankly hawapo tena.
Walimpenda ila wanaweza kumkimbia, walimthamini wataanza kumshusha, na ahadi ni deni. Muda unaondoka, na tusi kubwa kwa mashabiki wa Liverpool ni mara ya mwisho kutwaa ubingwa, na Klopp anashiriki dhambi kwa makusudi.

No comments:

Post a Comment