Ibrahimovic alifikisha jumla ya mabao 26 kwenye mashidano yote msimu huu baada ya kufunga mabao 2 kwenye ushindi wa mabao 3-2 kwenye fainali ya EFL dhidi ya Southampton kwenye uwanja wa Wembley huku bao lake la pili likiwa la ushindi.
Mchezaji huyo mwenye miaka 35 alisaini mkataba wa mwaka mmoja akiwa kama mchezaji huru akitokea katika klabu ya Paris Saint-Germain kwenye majira yaliyopita ya kiangazi huku mkataba wake ukiwa na ruhusa ya yeye kuongeza miezi 12 kulingana na uwezo atakounyesha.
Ibrahimovic ameshavuka vipimo na malengo yote aliyowekewa mpaka sasa na bado hajaonyesha ishara ya kuongeza mkataba.
Na huku Mourinho akitegemea mchezaji huyu kubaki United, hata kama klabu hiyo itasajili mchezaji mwingine kwenye majira yajayo ya kiangazi, anakiri kuwa nguvu ya mashabiki itasaidia zaidi.
“Huwa siombi,” Mourinho alisema. “Lakini kama itahitajika ama itabidi, inawezekana mashabiki wakatakiwa kwenda kwenye nyumba yake na kumwomba aweze kubaki kwenye klabu hii.
“Ni mchezaji mpuuzi pekee anayeweza kuja Uingereza akiwa na umri wa miaka 35 ijapokuwa tu kama anajisikia anaweza kufanya hivyo.
No comments:
Post a Comment