Sunday, February 26, 2017

Wachawi wapanga kumuondoa Trump madarakani


Kadi za uchawiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionKadi za uchawi
Wapinzani wengi wa rais wa Marekani Donald Trump, wanaamini kuwa itawabidi wasubiri kwa miaka minne ili aweze kuondoka madarakani.
Lakini wachawi nchini Marekani hawakubaliani na hilo.
Usiku wa manane siku ya Ijumaa, wale wanaoamini uchawi kote nchini Marekani, waliandaa matambiko yenye nia ya kumuondoa Trump uongozini.
Hadi sasa ukurasa wa Facebook wa matambiko huyo umepata wafuasi 10,500.
Ukurasa wa Facebook umebuniwa kuunga mkono uchawi huoHaki miliki ya pichaFACEBOOK/BINDTRUMP
Image captionUkurasa wa Facebook umebuniwa kuunga mkono uchawi huo
Hatua hizo zimezua ghadhabu kotoka kwa wakirsto ambao wamewalaumu wachawi hao wa kutangaza vita vya kiroho.
Wachawi hao wanapanga kurudia tambuko hilo hadi pale Trump atakapoondoka ofisini. Tambiko lingine litafanyika machi 26.
Chama cha wakiristo nacho kilitangaza tarehe 24 mwezi Februari kama siku ya maombi ya kuukabili uchawi huo.
Hata hivyo Trump hajazungumzia lolote kuhusu vita hivyo kati ya kanisa na uchawi.
Wafuasi wa TrumpHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWafuasi wa Trump

No comments:

Post a Comment