Sunday, February 26, 2017

Mashambulizi 10 hutokea kila siku dhidi ya wahamiaji Ujerumani


Mashambulizi dhidi ya sehemu wanamoishi wahamiaji ni mengiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMashambulizi dhidi ya sehemu wanamoishi wahamiaji ni mengi
Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa yametokea mashambulio zaidi ya 2500 dhidi ya wakimbizi nchini Ujerumani mwaka jana.
Watu zaidi ya 50 walijeruhiwa, wakiwemo watoto 43.
Mwaka 2016, ndio ulikuwa wa kwanza ambapo takwimu kama hizo zilianza kukusanywa.
Takwimu za wizara ya mambo ya ndani ya nchi, pia zinaonyesha kuwa vituo vya wakimbizi vilishambuliwa karibu mara elfu moja , sawa na mwaka uliotangulia.
Mwaka 2015, Ujerumani ilipokea wahamiaji karibu laki tisa.
Idadi ya wanaoomba hifadhi Ujerumnai ilipanda mwaka 2016

No comments:

Post a Comment