Sunday, February 26, 2017

Kiongozi wa Taliban awataka watu kupanda miti Afghanistan



Haki miliki ya pichaAP
Image captionWapiganaji wa TalibanWapiganaji wa Taliban

Kiongozi wa Taliban nchini Afghanistan Hibatullah Akhundzada amewashauri watu nchini humo kupanda miti zaidi.
Katika taarifa alitoa wito kwa raia na wapiganaji kupanda mti mmoja au zaidi kwa minajii ya kurembesha nchi.
Afghanistan inakumbwa na tatizo la ukataji miti, huku miti ikikatwa kwa kuni na biashara haramu ya mbao.
Si kawaida kwa Taliban kutoa taarifa zinazohusu mazingira.

Watu wengi nchini Afghanistan hutumia kuniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWatu wengi nchini Afghanistan hutumia kuni

Akhundzada, ambaye alitangazwa kiongzi mwezi Mei mwaka uliopita, anafahamika kama kiongozi wa kidini kuliko kiongozi wa kivita.
Taliban ushiriki zaidi na uzalishaji wa bangi ulioharamishwa nchini Afghanistan na hutosa ushuru maeneo ambayo wanadhibiti.
Kundi hilo lilitawala sehemu kubwa ya Afghanistan kuanzia mwaka 1996 hadi wakatai lilipinduliwa muungano ulioongozwa na Mareknai mwaka 2001.

Hibatullah Akhundzada ni msomi wa kidini kutoka Kandahar

No comments:

Post a Comment