Tuesday, February 28, 2017

Haki miliki ya pichaGOOGLE Image caption Timu Azania Group Timu ya Azania Group, ndiyo itakayowakilisha Tanzania katika mashindano ya kikanda ya Afrika Mashariki, ya Benki ya "Standard Chartered-Road to Anfield" yatakaofanyika uwanja wa Jakaya Kikwete Youth Park Jumamosi, Machi 4. Azania walipata ushindi huo kwa kuichakaza timu ya H&R Consultancy mabao ya 6-5 kwa penati dhidi ya katika mchezo wa kukata na shoka uliofanyika mwishoni mwa wiki na kufanikiwa kuipeperusha bendera ya Tanzania. Kwa maana hiyo, Azania Group wanatarajia kumenyana uso kwa uso na washindi wa michuano hiyo kutoka nchi za Kenya na Uganda. Washindi wa michuano hiyo nchini Uganda ni timu ya Cocacola wakati kidedea wa kombe hilo nchini Kenya ni Radio ya Capital FM.


Wachezaji wa timu ya Hull City nchini UingerezaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWachezaji wa timu ya Hull City nchini Uingereza
Bao la dakika za mwisho la Humphrey Mieno halikutosha kuwaokoa wachezaji wa timu ya Sport pesa kutoka Kenya ambao walilazwa na timu ya Hull City nchini Uingereza katika mechi ya kirafiki .
Bao la kujifunga la beki Harun Shakava katika kipindi cha pili liliigharimu Kenya ambayo ilikuwa imeahidiwa kitita cha shilingi milioni 1.1 iwapo wangeishinda timu hiyo ya Ligi ya Uingereza.
Hull City walikuwa juu kwa bao moja lililofungwa na Elliot Holmes katika dakika ya 11.
Kocha Stanley Okumbi alianzisha nyota wake wote huku mshambuliaji Allan Wanga akiongoza safu yake ya mashambulizi.
Waandalizi hatahivyo waliwasilisha wachezaji watano pekee kutoka kikosi cha kwanza Josh Tymon,Greg Olley,Max Sheaf,Greg Luer na Jarrod Bowen.
Daan Windas ambaye mchezo wake 2008 uliisaidia timu hiyo kupanda daraja alichezeshwa kama mchezaji wa ziada.

No comments:

Post a Comment