Image captionMuonekano wa uwanja wa Madeira kwa sasa
Licha ya kupoteza 2-1 dhidi ya Sweden Ronaldo ataondoka kwa ufahari nchini mwake baada ya uwanja wa ndege wa Madeira sehemu aliyozaliwa kubadiliwha njina na kuwa uwanja wa ndege wa Cristiano Ronaldo
Ureno walianza kupata goli baada ya mlinzi wa Sweden Andreas Granqvist kujifunga mwenyewe dakika ya 71.
Viktor Claesson akaiandikia Sweden goli la kwanza kabla ya Cavaco Cancelo kujifunga muda wa majeruhi.
Ronaldo anatarajiwa kuhudhuria sherehe za kuitwa jina hilo siku ya Jumatano.
Image captionRonaldo ni miongoni mwa wachezaji wenye historia ya kuvutia zaidi Ureno
Mchezaji huyo mwenye miaka 32 aliyeingoza timu yake ya taifa kutwaa kombe la mataifa ya Ulaya 2016, amezaliwa katika mji wa Madeira katika kitongoji cha Funchal, kabla ya kujiunga na timu ya Lisbon na baadaye Manchester United.
Baadhi ya wanasiasa wamepinga uamuzi wa kubadili jina la uwanja wa ndege wa Maderia kuitwa Cristiano Ronaldo Airport.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionMfano wa sarafu iliyoibwa
Sarafu kubwa iliyotengenezwa kwa dhahabu, ambayo ina picha ya Malkia Elizabeth wa Uingereza, ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya $4m (£3.2m), imeibiwa kutoka kwenye makumbusho Ujerumani.
Sarafu hiyo kutoka Canada imeandikwa kuwa ya thamani ya $1m, lakini kwa sababu imetengenezwa kwa kilo 100 za dhahabu, thamani yake ni ya juu sana kwa kutumia bei ya sasa ya dhahabu.
Iliibiwa usiku kutoka makavazi ya Bode mjini Berlin.
Haijabainika ni vipi wezi walifanikiwa kuingia bila kugunduliwa na mtambo wa kuzuia wezi, na kisha wakafanikiwa kutoroka na sarafu hiyo ambayo nusu kipenyo chake ni cha nusu mita.
Haki miliki ya pichaPAImage captionTheresa May akitia saini barua ya kuanza kujiondoa EU
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May ametia saini barua ambayo itaanzisha rasmi mchakato wa kuiondoa Uingereza kutoka kwa Muungano wa Ulaya.
Barua hiyo inatoa taarifa rasmi ya kujiondoa kwa muungano huo kwa kitumia Kifungu 50 cha Mkataba wa Lisbon.
Itawasilishwa kwa rais wa Baraza la Ulaya Donald Tusk baadaye leo.
Kwenye taarifa kwa bunge la chini nchini Uingereza, Bi May baadaye anatarajiwa kuwaambia wabunge kwamba hatua hiyo inaashiria "wakati we taifa letu kuungana pamoja."
Hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kura ya maoni iliyoandaliwa Juni mwaka jana, ambapo wapiga kura waliunga mkono kujiondoa kutoka kwa EU.
Barua ya Bi May itawasilishwa kwa Bw Tusk Jumatano mwenzo wa saa sita unusu adhuhuri saa za Uingereza na balozi wa nchi hiyo katika EU Sir Tim Barrow.
Waziri mkuu ambaye ataongoza kikao cha baraza la mawaziri asubuhi, baadaye atatoa hotuba rasmi kwa wabunge kuthibitisha kwamba mchakato wa Uingereza kujiondoa EU umeanza.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionBi May amewaomba watu walio Uingereza kuungana
Ataahidi "kuwakilisha kila mtu katika Uingereza yote" wakati wa mazungumzo hayo - wakiwemo raia wa EU (wanaoishi Uingereza), ambao bado haijafikiwa uamuzi kuhusu hatima yao baada ya Uingereza kujiondoa kutoka kwa muungano huo.
"Nimejitolea kuhakikisha tunapata mkataba bora zaidi kwa kila mtu katika nchi hii," anatarajiwa kusema.
"Kwani, tunapokabili fursa na changamoto zilizopo mbele yetu, maadili yetu ya pamoja, maslahi na ndoto zetu zinaweza - na ni lazima - zitulete pamoja."
Matukio makuu yanayotarajiwa
29 Machi, 2017 - UIngereza yaanza kutumia Kifungu 50
29 Aprili- Mkutano mkuu wa viongozi 27 wa EU (bila Uingereza) kuipa Tume ya Ulaya ruhusa ya kushauriana na Uingereza
Mei - Tume ya Ulaya kuchapisha mwongozo wa mashauriano kwa kufuata ruhusa kutoka kwa viongozi wa EU. EU inaweza kuzungumzia uwezekano wa mashauriano sambamba wa mkataba wa baadaye wa biashara kati ya UK na EU
Mei/Juni 2017 - Mashauriano kuanza
23 Aprili na 7 Mei - Uchaguzi wa urais Ufaransa
24 Septemba - Uchaguzi wa ubunge Ujerumani
Majira ya kipupwe 2017 - Serikali ya Uingereza inatarajiwa kutunga sheria ya kujiondoa EU na kuweka sheria zote zilizopo chini ya EU kuwa sehemu ya Sheria za Uingereza
Oktoba 2018 - Mashauriano yanatarajiwa kukamilika
Kati ya Oktoba 2018 na Machi 2019 - Mabunge ya Uingereza, baraza la Ulaya na Bunge la Ulaya kupigia kura mkataba utakaokuwa umeafikiwa
Kiongozi wa chama cha Alliance for Change & Transparency Wazalendo nchini Tanzania Zitto Kabwe amesema waziri wa habari aliyefutwa kazi Bw Nape Nnauye "ni shujaa".
Kwenye Twitter, Bw Kabwe, ambaye ni mbunge wa Kigoma-Ujiji Municipality amesema amewasiliana na Bw Nnauye ambaye amemthibitishia kwamba ni kweli ameondolewa kwenye wadhifa wake wa uwaziri.
Taarifa kutoka ikulu mapema leo ilitangaza waziri mpya wa habari, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuwa Dkt. Harrison George Mwakyembe.
Taarifa hiyo haikusema chochote kuhusu hatima ya Bw Nnauye.
Haki miliki ya pichaTWITTER
Dkt Mwakyembe amekuwa akihudumu kama Waziri wa Katiba na Sheria.
Bw Nnauye kwenye Twitter amewaomba watu kuwa na subira na kuahidi kwamba atazungumza na wanahabari baadaye leo.
"Ndugu zangu naomba TUTULIE! LEO mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba TUTULIE!" ameandika.
Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limempongeza Dkt Mwakwembe kufuatia uteuzi wake.
Bw Nauye amevuliwa majukumu yake siku moja baada yake kupokea ripoti ya kamati ya uchunguzi kuhusu uvamizi uliotekelezwa na mtu anayedaiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika studio za kituo cha habari cha kibinafsi cha Clouds mwishoni mwa wiki.
Image captionWaziri wa zamani wa habari aliyevuliwa madaraka Nape Nnauye
Kamati hiyo, kwenye ripoti yake, ilionekana kumkosoa Bw Makonda na kusema alitumia vibaya mamlaka yake.
Kamati hiyo ilipendekeza, miongoni mwa mengine, kwamba Bw Nnauye awasilishe malalamiko ya waandishi wa habari dhidi ya mkuu huyo wa mkoa kwa Rais wa Tanzania pamoja na kuanzishwa kwa uchunguzi dhidi ya polisi waliongia na silaha za moto kwenye chombo hicho cha utangazaji.
Akipokea ripoti hiyo, Bw Nnauye pamoja na kuwataka viongozi wa umma kufanya kazi kwa uweledi, aliahidi kukabidhi taarifa hiyo kwa mamlaka za juu zaidi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kutokana na mapendekezo yaliyomo katika taarifa hiyo.
Dkt Magufuli ameonekana kufurahishwa na utendakazi wa Bw Makonda na mara kwa mara amesifu hatua alizochukua.
Rais John Magufuli alisema katika hotuba yake Jumatatu alipokuwa akizindua ujenzi wa barabara ya juu eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam kuwa Bw Makonda aendelee kuchapa kazi na kwamba yeye hafanyii kazi maneno ya kwenye mitandao kwa sababu yeye ndiye rais wa nchi.
Image captionDkt. Harrison George Mwakyembe awali alikuwa waziri wa sheria sasa ni waziri wa habari
Dkt Magufuli alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanaingilia majukumu yake wakati yeye ndiye mwenye uamuzi na kwamba hapangiwi kazi ya kufanya kwa sababu anajiamini.
Prof Kabudi, ambaye ameteuliwa kuwa waziri mpya wa katiba na sheria aliteuliwa Januari mwaka huu kuwa mbunge mteule.
Image captionAwali Prof. Palamagamba Aidan Kabudi alikuwa mhadhiri wa chuo kukuu cha Dar es salaam na sasa ameteuliwa kuwa waziri wa sheria
Yeye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria na alikuwa mmoja kati ya wajumbe wa Tume ya Kukusanya na Kuratibu Maoni ya Katiba, iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu Joseph Warioba.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionFrancois Fillon
Mgombea kiti cha urais nchini Ufaransa Francois Fillon, sasa anachunguzwa rasmi kwa tuhuma kwamba alimfanyia mipango mkewe muingereza, alipwe mshahara kwa kazi ya usaidzi katika bunge.
Fillon anakana madai hayo na kudai ataendelea na kampeni za uchaguzi huo wa mwezi ujao.
Bwana Fillon anadaiwa kumlipa mkewe na wanawe wawili kazi iliyokuw ifanywe bungeni lakini haikufanywa madai ambayo wote wanakanusha.
Wakati mmoja Fillon alisema kwamba atajiuzulu kama mgombea wa chama cha Republican iwapo atachunguzwa rasmi lakini baadaye alibadili msimamo huo.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionFrancois Fillon
Mgombea kiti cha urais nchini Ufaransa Francois Fillon, sasa anachunguzwa rasmi kwa tuhuma kwamba alimfanyia mipango mkewe muingereza, alipwe mshahara kwa kazi ya usaidzi katika bunge.
Fillon anakana madai hayo na kudai ataendelea na kampeni za uchaguzi huo wa mwezi ujao.
Bwana Fillon anadaiwa kumlipa mkewe na wanawe wawili kazi iliyokuw ifanywe bungeni lakini haikufanywa madai ambayo wote wanakanusha.
Wakati mmoja Fillon alisema kwamba atajiuzulu kama mgombea wa chama cha Republican iwapo atachunguzwa rasmi lakini baadaye alibadili msimamo huo.