Friday, May 12, 2017

Trump: Sichunguzwi na FBI

Rais Trump anasema kuwa hachunguzwiHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionRais Trump anasema kuwa hachunguzwi
Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kwamba hafanyiwi uchunguzi wowote baada ya kumfuta kazi mkurugenzi wa shirika la ujasusi la FBI.
Bwana Trump aliambia chombo cha habari cha NBC kwamba ilikuwa uamuzi wake pekee kumsimamisha kazi James Comey.
Bwana Comey alikuwa akiongoza uchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani uliokamilika mbali na uwezekano kwamba kulikuwa na mawasiliano kati ya, maafisa wa Trump na Urusi wakati wa kampeni.
Bwana Trump ameutaja uchunguzi huo kuwa unafiki mkubwa madai yaliopingwa na Mrithi wa Comey.
Katika mahojiano yake ya kwanza tangu alipomfuta kazi mkurugenzi huyo , Bwana Trump aliambia NBC siku ya Alhamisi kwamba alimuuliza bwana Comey iwapo alikuwa akimchunguza.
Nilimwambia iwapo inawezekana unaweza kuniambia, Je Ninachunguzwa? Aliniambia ,huchunguzwi.
''Najua sichunguzwi'', Bwana Trump alimwamabia aliyekuwa akimhoji, akirejelea madai aliyotoa katika baraua ya Jumanne ya kumfuta kazi bwana Comey.
Rais huyo pia alipinga maelelezo ya ikuu ya Whitehouse kwamba alimfuta bwana Comey baada mapendekezo kutoka maafisa wakuu wa wizara ya haki.

Thursday, May 11, 2017

Mkurugenzi wa kampuni ya ndege apigwa chapati ya uso Australia

Haki miliki ya pichaSEVEN NEWS
Image captioniHotuba ya mkurugenzi wa shirika la ndege la Australia Airline Qantas ilisitishwa kwa muda baada ya kupigwa na chapati usoniQantas ilisitishwa kwa muda baada ya kupigwa na chaHotuba ya mkurugenzi wa shirika la ndege la Austraa Airline lpati usoni
Hotuba ya mkurugenzi wa shirika la ndege la Australia Airline Qantas ilisitishwa kwa muda baada ya kupigwa na chapati usoni.
Alan Joyce alikuwa akihutubia mkutano wa biashara katika eneo la Perth wakati mtu mmoja alipopanda jukwaani na kumpiga chapati ya uso.
Mtu huyo alikamatwa na maafisa wa usalama .
Maafisa wa polisi wanasema kuwa wanamuhoji.
Bwana Joyce alikuwa akizungumza kuhusu hatua ya safari ya moja kwa moja kutoka London hadi Perth bila kusimama katika vituo vilivyopo.
Alan Joyce wa shirika la ndege la Australian QantasHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAlan Joyce wa shirika la ndege la Australian Qantas
''Sijui hilo lilisababishwa na nini '',aliwaambia takriban watu 500 waliokuwa wakisikiliza hotuba yake.
Bwana Joyce aliondoka katika jukwaa hilo kwa muda ili kusafisha uso wake kabla ya kurudi akishangiliwa.
''Sasa iwapo kuna chapati nyengine tafadhali malizeni shughuli yake'', alisema.

China yajiandaa kutuma binadamu wakaishi kwenye Mwezi

Mwezi na bendera ya ChinaHaki miliki ya pichaAFP
China imepiga hatua nyingine katika mpango wake wa anga za juu, baada ya kuanza kufanyia majaribio mpango wa kupeleka binadamu wakaishi kwa muda mrefu kwenye Mwezi.
Wanafunzi wa sayansi wamehamia katika chumba maalum chenye mazingira yanayofanana na ya Mwezi ambapo watakaa kwa siku 200.
Lengo ni kuwaanda kwa safari ya kuishi kwa muda mrefu kwenye kituo cha anga za juu kwenye Mwezi, bila kupokea usaidizi wowote kutoka ardhini.
China imewekeza pesa nyingi sana katika mpango wake wa anga za juu, ikilenga kushindana na Marekani an urusi.
Wanafunzi wanne wa taaluma ya anga za juu wanaosomea shahada za juu chuo kikuu cha beihang walihamia chumba hicho maalum Jumatano, ambacho kimepewa jina Yuegong-1. Maana ya jina hilo ni Kasri la Mwezi.
Watakaa katika chumba hicho maalum kwa siku 60, lakini watafuatiwa na kundi jingine la wataalamu ambao watakaa kwa siku 200 mfululizo.
Wanne hao kisha watarejea na kukaa kwa siku 105.
Shirika la habari la Xinhua linasema miongoni mwa mambo yanayofanyiwa majaribio ni uwezekano wa kuishi kwa kujitosheleza anga za juu kwa muda mrefu bila kutegemea msaada kutoka nje.
Mwaka 2016, wana anga wa China Jin Haipeng (kulia) na Chen Dong walikaa siku 30 anga za juuHaki miliki ya pichaAP
Image captionMwaka 2016, wana anga wa China Jin Haipeng (kulia) na Chen Dong walikaa siku 30 anga za juu
Kinyesi cha binadamu kitaozeshwa kwa kutumia viumbe hai.
Mimea na mboga itakuzwa kwa kutumia taka mbalimbali za chakula na matumizi mengine.
Mpango wa kutuma watu wakakae muda mrefu kwenye Mwezi utajumuisha kutumwa kwa sehemu mbili kubwa za mtambo za kukuzia mimea, na sehemu nyingine kubwa sawa na nyumba ambao itakuwa na vyumba vinne vya kulala, sebule moja, bafu, chumba cha kubadilishia taka na chumba cha kufugia wanyama.
Ingawa mpango huo wa Kasri la Mwezi unawaandaa wana anga kukaa muda mrefu kwenye Mwezi, kwa sasa China haijapanga kutuma wana anga wengine kwenye Mwezi kabla ya miaka 10 kupita.

Mugabe huwa anapumzisha macho si kulala

Bw Mugabe akiwa mkutanoni Afrika Kusini wiki iliyopitaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBw Mugabe akiwa mkutanoni Afrika Kusini wiki iliyopita
Msemaji wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kiongozi huyo huwa anapumzisha macho tu na si kulala wakati wa mikutano kama wanavyoamini watu wengi.
Kiongozi huyo amekuwa akionekana kusinzia katika mikutano mingi.
"Rais huwa anasumbuliwa na mwanga mkali," George Charamba amenukuliwa akisema na gazeti la serikali la Herald.
Rais huyo kwa sasa yupo nchini Singapore akipokea matibabu maalum kwenye macho yake.
Bw Mugabe, 93, anapanga kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.
"Huwa najihisi kama mtu ambaye amekosa kutekeleza kazi yake vyema ninaposoma (kwenye vyombo vya habari na mtandaoni) kwamba rais alikuwa anasinzia katika makongamano - la hasha," Bw Charamba amesema.
Alilinganisha tatizo la Bw Mugabe na matatizo ya macho ambayo yalikuwa yanamsibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Bw Mandela alikuwa anatatizwa na mwanga mkali na wapiga picha hawakuruhusiwa kutumia mwanga wa kamera wakati wanapiga picha katika hafla zake.
Matatizo ya Bw Mandela yalitokana na kufanya kazi kwa muda mrefu katika timbo na pia kufungwa jela muda mrefu Robben Island.
Mugabe Bamako Januari 13, 2017.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMacho ya Robert Mugabe hutatizwa na mwanga, msemaji wake amesema. Hapa Mugabe anaonekana akiwa Bamako Januari 13, 2017.
Safari za Bw Mugabe za mara kwa mara nje ya nchi zimekuwa zikishutumiwa sana na wakosoaji wake.
Sekta ya afya nchini Zimbabwe imedorora na wahudumu wa afya hulalamika kwamba huwa hawalipwi vyema.

Ukuta wawaua wageni 22 harusini India

Ukuta ulioanguka na kuwaua wageni 22 harusini IndiaHaki miliki ya pichaBANWARI UPADHYAY
Image captionUkuta ulioanguka na kuwaua wageni 22 harusini India
Takriban watu 22 wamefariki baada ya ukuta kuwaangukia wakati wa harusi kaskazini mwa India.
Wageni hao walikuwa wamejikinga na mvua kubwa inayoendelea kunyesha kabla ya ukuta huo kuwaangukia.
Watu wengine 26 walijeruhiwa katika jali hiyo ya Bharatpur ,wilaya moja ya jimbo la Rajasthan ,15 kati yao wakiwa na majeraha mabaya.
Vyombo vya habari vinasema kuwa vibanda vya kuuza chakula vilikuwa vimewekwa kandakando ya ukuta huo karibu na harusi.
Ukuta huo na kibanda ulianguka kutokana na kimbunga kulingana na afisa wa Polisi Anil Tank aliyenukuliwa akisema.
Alisema kwamba ukuta huo wenye urefu wa futi 90 uliwaangukia wageni wengi.
''Waliojeruhiwa walikimbizwa katika hospitali za eneo hilo mara moja huku wakipewa matibabu''.

China yailalamikia Korea Kusini kuhusu mtambo wa Marekani

Mtambo wa Thaad umewekwa kuzuia makombora kutoka Korea KaskaziniHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMtambo wa Thaad umewekwa kuzuia makombora kutoka Korea Kaskazini
Rais wa Uchina amelalamikia hatua ya Marekani kuweka mtambo wa kuzuia makombora nchini Korea Kusini.
Rais Xi Jinping amepinga kuwepo kwa mtambo huo katika mazungumzo yake ya kwanza na rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in.
Mtambo huo wa Thaad, ambao lengo lake ni kutungua makombora ambayo huenda yakarushwa na Korea Kaskazini, ulianza kufanya kazi wiki iliyopita.
Beijing hata hivyo inasema mtambo huo unaweza kutumiwa na Marekani kufanya upelelezi katika maeneo ya China na imeupinga sana.
Uhusiano kati ya Beijing na Seoul umeathirika sana kutokana na kuwekwa kwa mtambo huo.
Bw Moon alichaguliwa kuwa rais mpya wa Korea Kusini siku ya Jumanne.
Anakabiliwa na changamoto ya kusawazisha uhusiano kati ya nchi hiyo na Marekani, mshirika wa tangu zamani wa Seoul, pamoja na uhusiano wake na China - ambayo anahitaji usaidizi wake kukabiliana na Korea Kaskazini na mpango wake wa kuwa na silaha za nyuklia.
Msemaji wa rais wa Korea Kusini alsiema kiongozi huyo wa China, ambaye ndiye aliyepiga simu, alieleza sabbau za "Beijing kupinga kwa dhati" kuwepo kwa mtambo huo wa kuzuia makombora.
Shirika la habari la serikali ya Korea Kusini Yonhap limemnukuu msemaji huyo Yoon Young-chan akisema: "Rais Moon amesema suala kuhusu Thaad linaweza likatatuliwa iwapo hakutakuwa na uchokozi tena kutoka kwa Korea kaskazini."
Bw Moon pia aliibua suala la kulipiza kisasi dhidi ya kampuni za Korea Kusini nchini China.
Marekani ilisema tambo huo wa Thaad ulianza kufanya kazi Korea Kusini Mei 2 Seongju, South Korea, 26 April 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarekani ilisema tambo huo wa Thaad ulianza kufanya kazi Korea Kusini Mei 2
Amesema atatumba ujumbe Beijing kujadiliana na maafisa wa China kuhusu Korea Kaskazini na mpango huo wa Thaad.
Kuwekwa kwa mtambo huo wa Thaad kuliidhinishwa na mtangulizi wa bw Moon, Park Guen-hye ambaye kwa sasa yumo gerezani akisubiri kusikizwa kwa kesi yake kuhusu tuhuma za ufisadi.
Msimamo wa Bw Moon kuhusu Thaad haufahamiki vyema lakini ameonekana kutokuwa na msimmao thabiti awali.
Baadhi ya wakazi Korea Kusini waliandamana kupinga kuwekwa kwa mtambo huo 28 Aprili 2017.Haki miliki ya pichaEPA
Image captionBaadhi ya wakazi Korea Kusini waliandamana kupinga kuwekwa kwa mtambo huo
Msemaji wake alishtuumu uamuzi wa Marekani kuweka mtambo huo wiki chache kabla ya uchaguzi, akisema hilo lilizuia serikali ambayo ingechaguliwa kupata fursa ya kufanya uamuzi kuhusu mtambo huo.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa China amesema pande zote mbili zimeeleza nia ya "kuimarisha tena uhusiano kati ya nchi hizo mbili".
Bw Moon na Bw Xi waliafikiana kwamba nchi zote mbili zina lengo la pamoja na kuhakikisha Korea Kaskazini haina silaha za nyuklia.
Bw Moon amekuwa akitaka mazungumzo yatumiwe kutatua mzozo huo, jambo ambalo linatofautiana na mtangulizi wake aliyechukua msimamo mkali zaidi.

THAAD ni nini?

  • Ni teknolojia ya kujilinda ya kutungua makombora ya masafa mafupi na wastani ambayo huyaharibu yanapokaribia kulipuka.
  • Hugonga kombora la kuliharibu
  • Ina uwezo wa kufika umbali wa kilomita 200 na inaweza kurushwa juu hadi kilomita 150 angani
  • Marekani imewahi kuweka mitambo kama hiyo Guam na Hawaii kujilinda dhidi ya uwezekano wa mashambulizi kutoka kwa Korea Kaskazini
Thaad missile defence system graphic
Image captionMtambo huo hufanya kazi kwa kutungua makombora ya adui
Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
Image captionUwezo wa makombora ya Korea Kaskazini
Ramani ya South Korea

Majaribio ya ndege mpya za Boeing yasitishwa

Boeing 737 MAXHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Shirika la ndege la Boeing limesitisha kwa muda safari za kufanyia majaribio ndege yake mpya ya 737 MAX kutokana na uwezekano wa kasoro kwenye injini za ndege hizo.
Hatua hiyo imechukuliwa siku chache kabla ya shirika hilo la ndege lenye makao yake Marekani kuwasilisha ndege za kwanza kwa mteja.
Lakini Boeing wamesema wataendelea na mpango wake wa kuanza kuwasilisha ndege hizo za MAX kwa wateja baadaye mwezi huu, na kwamba kampuni hiyo itaendelea kuunga ndege hizo kama kawaida.
American Airlines, Southwest, na shirika la Shandong Airlines la China ni miongoni mwa mashirika ambayo yameagiza ndege hizo.
Mapema mwaka huu, shirika la ndege la SpiceJet kutoka India liliwasilisha ombi la kununua ndege 205 mpya kutoka wka Boeing, ununuzi huo ukitarajiwa kuwa wa thamani ya $22bn (£18bn). Boeing wamesema ndege za kwanza za Max 737 zitawasilishwa kwa SpiceJet mwaka 2018.
Ndege za MAX zimeundwa kutotumia sana mafuta na zimeundwa kuchukua nafasi za ndege muundo wa 737 za awali, ambazo ziliuzwa kwa wingi sana na kampuni hiyo.
Boeing wanasema walifahamishwa wiki iliyopita kwamba huenda kuna kasoro kwenye injini za ndege hizo ambazo zilitengenezwa na kampuni ya kimataifa ya kuunda sehemu za injini ya CFM International.
CFM ni kampuni inayomilikiwa kwa pamoja na kampuni ya Marekani ya General Electric (GE) Safran ya Ufaransa na ndiyo iliyopewa kazi ya kuunda injini za ndege hizo za 737 Max.
Boeing wamesema hawakuwa wamepata taarifa zozote za hitilafu kwenye injini awali wakati was aa 2,000 za safari za majaribio.
Boeing 737 Max 9 taking offHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBoeing 737 MAX 9 ilifanya safari yake ya kwanza Aprili
Ndege hiyo ya 737 MAX 8, inauzwa $110m lakini mashirika mengi ya ndege sana hupokea kipunguzo cha bei.
Muundo utakaofuata wa ndege hizo, 737 MAX 9, utakuwa na uwezo wa kubeba abiria wengi.
Kampuni ya Boeing ilisherehekea miaka 100 tangu kuanzishwa kwake mwaka jana.